DARASA LA ALHAMISI NA DR. CHRIS MAUKI: JINSI YA KUSHUHULIKIA LAWAMA NA WALAUMU

JINSI YA KUSHUHULIKIA LAWAMA NA WALAUMU

 

Hakuna hata mmoja anayependa kupokea lawama. Na mara nyingi jinsi unavyomjibu yule anayekulaumu sio katika hali njema, labda utamwambia maneno ya dharau kejeli, matusi au kujibu kihasira. Kibaya zaidi ni kwamba majibu haya yote hayampoozi mlaumu, kinyume chake yana mpa moto wa kuendelea kulaumu, na hivyo hali kuwa mbaya zaidi.

Katika hali zote lawama zinakatolewa kuna kiwango Fulani cha upande mmoja kuhisi kutotendewa sawa, ingawa mara nyingine lawama hizi huelekezwa kwa asiye mhusika.

Wengi hupenda kuzirusha lawama kwa wale walio dhaifu kwao, mf. Baba kumlaumu mama, mama kulaumu watoto au wafanyakazi nk.

Mara nyingi ni  ngumu kunyamaza pale unaporushiwa lawama, hususani pale unapojua kabisa kuwa lawama hizo hazikuhusu wewe, ila yakubidi ujitahidi kukaa kimya, kwa sababu muhimu zifuatazo.

  1. Kama wote mtafuk moto na kuwajeuri hakuna kitakachofanyika hali itakuwa ngumu zaidi na mlaumu au mlalamishi atapata kitu kingine cha kulaumu juu yako.
  2. Kwa vyovyote lawama zitakavyokuwa, fahamu tu kuwa mteja (ikiwa ni kwenye biashara) wakati wote ana haki, fahamu hakuna biashara bila huyo mteja. Hata kama amekosa, mlaumu wakati wote hujiona ana haki ya kutoa malalamiko yake na kusikilizwa. Kwa kunyamaza na kumsikiliza, unatunza kazi yako na kuiendeleza.
  3. Kama kelele hazitapungua, lawama zaweza kuvuka mpaka wa lawama za awali na kuwa lawama kwa mtu binafsi n ahii yaweza kuleta ugomvi binafsi.
  4. Kwa sababu ni rahisi sana kupandishwa hasira zaidi ya kupooza hasira, ikiwa utamruhusu mlaumu akupandishe hasira, utalazimika kuzielekezea hata kwa mwatu wengine wasio husika, ambazo unahitaji kuwa huduma pia. Hii sio haki na inawapa mlango mwingine wa kulaumu.
  5. Ukiruhusu mtu akupandishe hasira, kiwango chako cha msongo wa mawazo kitapanda, na hivyo waweza kujikuta unapata matatizo kiafya. Mf. Kuumwa kichwa mara kwa mara, mgongo kuuma, mshtuko wa tumbo, na mapigo ya moyo kuzidi kasi. BP, wale wenye vidonda vya tumbo huzidi kuuma nk.
  6. Kuruhusu kupandiswa hasira mara kwa mara kazini, huwafanya wengi kwenda kuzishushia nyumbani, nah ii huleta mfarakano na watu wa kwenye familia. Hasira na migongano hii ikizidi nyumbani, kasi utalala na kuamka nayo na hivyo kwenda nayo kazini asubuhi, hii ukufanya kuanza siku na hasira na hivyo kukuaruzana na yeyote yule.
  7. Unajua kabisa kuwa, sio jukumu lako kukasirikiak kazini dhidiya mteja au wateja wako au wale unao wahudumia, hali hii ikitokea, utajihisi vibaya moyoni, na waweza wapoteza hata wale ulionao karibu na walio marafiki.

 

NINI TUFANYE KWA MTU MWENYE TABIA YA LAWAMA

Jitahidi kujiweka huru mpole na asiyepaniki kwa vyovyote iwezekanavyo (be as relaxed as possible) vuta mwizi ndefu, acha mabega na shingo yako iwe huru mbali na hasira, hisi utulivu.

Tulia hadi joto na moto wa mlaumu ushuke, ukijaribu kuweka neno hapa, utatulia na kukuamkia tena. Mwili wako uonyeshe mawasiliano, weak pozi la utulivu sio la shari, muangalia machoni, usimkwepe, kama ni kwenye meza, egemea kidogo upande wake kama vile uko tayari kumsikiliza kwa upole.

Msikilize anachosema sawia, ikiwezekana chukua karatasi na kalamu akuone ukiandika pointi za kile anachalaumu. Hii itakusaidia kumwonyesha kuwa unamaanisha na hivyo kushuhulikia kile anacholaumu. Pia itakukumbusha wewe nini haswa kilikuwa kinalaumiwa mara baada ya yeye kunyamaza.

Baada ya kusikiliza anachokisema, mwonyeshe mlaumu kuwa unahisi sawa na vile anavyojisikia, na hata ingekuwa wewe ungeumia au ungelaumu. Mf. Mwambie “Naelewa kabisa jinsi ilivyokuudhi hasa jinsi ulivyochelewa kupata huduma” hii inamwonyesha, unamuhurumia na kwamba huoni kuwa analaumu tu bila sababu.

Pata muda wa kuliangalia tatizo sio mara zote mlaumu ana haki, ingawa huitaji kumwambia usoni. Kama ni jambo litakalohitaji muda basi mwombe muda wa kulishuhulikia na muahidi kumpa taarifa baadaye na kweli ufanye hivyo.

Pale unapogundua unakosa  au kampuni ndiyo  inatatizo katika lile lililokuwa lina laumiwa, basi omba radhi na uwe mkweli usitake kufunika na kujitetea.

Kamwe usijitetee, hatakama sio wewe mhusika mfa. “Sio kosa langu” mimi sikuwepo jana” kamwone bosi basi “Usilaumu kabla ya kuuliza kwanza” nk. Mlaumu hana muda wa kujua nani ni mhusika. Ukitupia lawama kwa wengine basi  unafanya wateja au mteja kupoteza imani na ofisi au wafanyakazi.

Kinachotakiwa, fanya kile uwezacho kupunguza tatizo, na mlaumu akuone ukiwabize kulifanya hilo. Mara utakapo mweleze kuwa unafanya kitu basi akuone ukikifanya muda huo.

Usishangae, hata mtu unaemjua kuwa ni mpole, anaweza kuwa mkali mara tu anapogeuka kulaumu, na hasa kama sio mara ya kwanza kwa tatizo la jinsi hiyo kutokea. Ni ngumu kuanza tu kushuhulikia kila anachokilaumu kabla kwanza hauja shuhulikia hisia zake. Sungumza nae kwanza. Mruhusu amalize kuongea ili apoe. Tingisha kichwa taratibu kuonyesha uko nay eye, akimaliza ongea taratibu.

Katika hali hii, yakupasa ujitahisi kuwa mpole, hata kama hiyo simu inaingilia mambo na ratibu zako najua hii ni ngumu hasa ukizingalia mlaumu hakuachii nafasi ya kumsikiliza anafuka tu kama moto.

Weka kalamu na karatasi karibu na wewe mara zote (kama ni ofisini) akiacha nafasi kidogo, muulize jina lake na ikibidi anapiga simu kutoka wapi, au ofisi gani, kama huna uhakika mwambie akutajie tarakimu za jina lake au la ofisi.

Kama kuna kitu utalazimika kuangalia katika mafaili, vitabu au computer, basi muulize kama angependelea kusubiria katika simu au kukata simu na umpigie baada ya muda jioni.

Kamwe usiweke mkono katika kisemeo (ikiwa ni simu ya mezani) mlaumu atahitimisha kwamba umeamua kumfanyia ukatili. Hii ni kwa sababu simu za sasa zimetengenezwa katika hali ambayo sauti inapita sawa katika sehemu ya kuzungumza na sehemu ya kusikilizia.

Ikiwa unataka kumkatisha mlaumu, wakati wote. Jaribu kumwita kwa jina lake, hii itamfanya atulie kukusikiliza zaidi ya kusema “samahani” “unajua”, ni kweli.

Kama ni kitu ambacho hautaweza kukishuhulikia muda huo, nae muda Fulani, jitahidi kuwa mwaminifu katika ahadi yako na atarajie majibu ya kutia moyo.

Mpe jina lako, pia, ili ajue ninaniwa kuwasiliana nae ikiwa atahiraji kupiga simu tena. Hii itamjengea imani ya kuwa, unamaanisha kumsaidia. Hata kama bado mambo hayajamalizika basi umpigie katika muda ulioahidi ili kumpa ripoti ya kunachoendelea. Kama hautaweza kulishuhulikia wewe, basi muahdi kumpa mtu muafaka, nawe uwekatibua kuakikisha madai yake yanatekelezwa.

Labda kosa laweza kuwa lako, ikiwa hivi, basi kubali na kumtake radhi, jaribu kumwelezea jinsi utakavyojitahidi kuweka mambo sawa, kamwe usijitetee wala kutupia lawama kwa wengine. Hali hii itakufanya uonekane dhaifu na mwepa majukumu. Unapokubali na kushuka mara nyingi mlaumu nae huelewa.

Ikiwa unaona lawama zinakuwa kubwa na kushindwa kuitafutia ufumbuzi haraka basi tafuta eneo au upenyo maafikiano hii itafanya kasi ya ujeuri wa mlaumu kupungua. Ni ngumu kuendelea kupigizane kelele na mtu anae afiki kila usemalo.

 

LAWAMA KWA NJIA YA SIMU

Lawama za nji hii huwa zaidi katika ulimwengu wa biashara, lawama hizi huleta matatizo mengi zaidi.

Watu wengine ambao hawawezi kulaumu uso kwa uso, huwa rahisi kwa kutupa lawama kupitia simu.

Katika biashara, au maofisini, hali huwa ngumu zaidi maana, unakuta mlaumu kashapiga simu kwa secretari (katika muhtasi) naye akawaruhusu waongee nawe, basi wanakuja na hasira mara dufu. Kama secretari sio mchapakazi na labda amechelewa kumuunganisha mlaumu huyu na wewe basi mlaumu anaweza kutka kukupasukia mara anapokupata.

Watu wengi huchemka zaidi kwenye simu zaidi ya ana kwa ana, hali hii hufanya maelewano kuwa magumu.

Kwa sababu hauwezi kuona sura yake wala mwili wake ni vigumu mmoja wenu kupa maana haujui jinsi anavyojielezea au mjinsi gani anammanisha kutafuta suluhu.

 

Na: Dr. Chris Mauki

Mtaalam wa saikolojia na mahusiano

University of Dar es salaam

0713 407182

Chrismauki57@gmail.com

www.chrismauki.com

 

 

 

 Dr. Chris Mauki. An expert in Relationships, Social and Counseling Psychology. Lecturer in Psychology: UDSM. Inspirational & Motivational speaker. Family man


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *