DARASA LA ALHAMISI NA DR. CHRIS MAUKI: IFAHAMU NGUVU ILIYONDANI YA MWANAMKE “Mtazamo wa Kisaikolojia”

IFAHAMU NGUVU ILIYONDANI YA MWANAMKE

“Mtazamo wa Kisaikolojia” 

 1. Mwanamke kwa mtazamo wa Mfalme Suleiman (Mith: 31:10, 20 – 30)
 • Wahitaji, ndugu na wasiondugu huponea kwake
 • Yeye ndio chanzo cha ndugu wa mume na wakwake kupatamani nyumbani kwake
 • Yeye ndiye mwenyekuleta mvuto wa nyumba yake.
  • Sebule hutoa picha halisi ya mama wa nyumba
 • Yeye ndiyo taa ya kujulikana kwa mume wake
  • Siku hizi mke anaweza kujulikana kupita mume.
  • Na anapoluwa huko nje hujivunia mkewe. (28a,b)
 • Ndiye nguzo ya uchumi wa nyumba (mst. 24).
  • Hali chakula cha uvivu, ni mchapa kazi na mbunifu
 • Ndiye nguzo ya mume na hekima ya nuymba
  • Humsaidia baba wa nyumba kimaamuzi (25)
 • Ndiye kisima cha nidhamu kwa watoto, ndiye model wa watoto.
 • Wamama hudharaulika sana siku hizi (28)
 • Huwa chanzo cha sifa kwa jamii na majirani
  • Familia hudharauliwa sio kwa anayoyafanya baba bali yale ayafanyayo mama, mfano; utaskia watu wakisema “ameharibiwa na mama yake” waswahili husema “ asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na dunia”Yeye ndiye mlinzi wafamilia (21)

2. Mwanamke kwa mtazamo wa kisaikolojia

a) Mwanamke ana uwezo wa kuona na kugundua yaliyo mbeleni.

 • Ndoto za kweli
 • Maono
 • Kuhisi hisia za mtu (mapema)

      b) Mwanamke ananguvu ya ajabu katika kinywa.

Neno dogo kutoka kinywani mwake laweza kuleta madhara.  Wakati  mamlaka  ya mwanaume yako katika   nguvu na kifua alichonacho  mamlaka na nguvu za mwanamke ziko ulimini mwake.

     c) Mwanamke ndiye amekabidhiwa jukumu la kuendeleza uumbaji

 • Usikae tu kuumba watoto, viko vitu tele vya kuumba. Umba mafanikio, umba uhalisi wa vile mbavyovitamani kwa mfano. afya, maendeleo ya watoto wako, hali ya mume wako, mashamba, mifugo, miradi nk.
 • Usiruhusu ibilisi kuharibu mimba za vitu ulivyoanza kuviumba
 • Angalia tofauti ya familia ya Baba Aliyeokoka tu, au mama aliyeokoka.

    d) Mwanamke ana nguvu ya ushauwishi.

 • Kumbuka mfano wa Esta na Modekai, Delila na Samsoni
 • Wanaume wangegundual hili wangepata upenyo kwenye mambo mengi. Wange weza kuwatumia wake zao katika kushawishi baadhi ya hoja na mipango ya kimaendeleo
 • Angalia katika makampuni, idadi ya wafanyakazi katika idara za rasilimali watu, masoko na mauzon.k wengi ni wanawake na ni kwaajili ya nguvu ya ushawishi waliyonayo. Angalia pia matangazo mbalimbaliu ya biashara uone ninani wahusika wakuu.

    e) Wanawake wanauwezo wa kustahimili magumu zaidi kulikowanaume. Kama vile njaa, maumivu, majaribu, na hata makadirio yao ya miaka ya kuishi (life expectancy) ni juu zaidi.

    f) Wanawake wana uwezo wa juu zaidi katika kufanya majadiliano ya manunuzi (high bargaining power)

NINI VIZUIZI VYA NGUVU HIZI KUFANYA KAZI?

 • Matumizi  mabaya ya kinywa/ulimi. Wanawake wanaongoza kwa kutofikiri kabla ya kusema, kesi na lawama nyingi kwa wanawake ni katika kile walichokisema wakati kwa wanaume ni katika kile walichokifanya. Wanawake wengi wamejutia matunda ya vinywa vyao. Wengi wametawanya, wameumiza na hata kuua kwasababu ya vinywa vyao.
 • Wengi wametumia vibaya nguvu ya ushawishi walionao. Mfano katika kugawanya watoto baina ya bande za wazazi, Kungangania wapenzi au wenza wasiokuwa wao. Wako hata walioangusha watumishi, kwakujua au kwa kutokujua
 • Kutojitambua kama mwanamke na uthamani alionao. Mfano kutokujua uwezo wa uumbaji wako, uwezo wa kuzuia maombi ya mumeo.

 

Imeandikwa na:

Chris Mauki

Mhadhiri na mshauri wa Saikolojia

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 Dr. Chris Mauki. An expert in Relationships, Social and Counseling Psychology. Lecturer in Psychology: UDSM. Inspirational & Motivational speaker. Family man


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *