MAMBO MUHIMU YAKUZINGATIA ILI KUBORESHA MAHUSIANO
Tunaposema mahusiano tunamaanisha
- Mahusiano baina ya marafiki wa jinsia moja
- Mahusiano baina ya wanafamilia
- Mahusiano baina ya wafanyakazi wa ofisi moja
- Mahusiano baina ya mzazi na mtoto
- Mahusiano baina ya mwajiri na mwajiriwa
- Mahusiano baina ya wapenzi, nk
- Kuwepo na upendo thabiti
– Upendo huvumilia/hauhusudu/hauhesabu mabaya/haujivuni
huvumilai yote, huamini yote.
Wawezaje kujijua kuwa tayari uko kwenye penzi
- Uhuru na uwazi wako katika kumwelezea mwenzako juu ya maishayako ya nyuma,hisia zako, matarajio yako, unavyovipenda na usivyovipenda
- Uwezo na utayari wa kutumia muda mrefu pamoja
Muda: Muda maranyingi unaweza kutumika kama kipimo kizuri cha pendo, jinsi mnavyokuwa na muda mchache ndivyo jinsi penzi lenu linavyonyauka, na jinsi mnavyo kuwa na muda mwingi ndivyo mnavyolikuza penzi lenu.
- Mawasiliano
Ukosefu wa kujua namna ya kuwasiliana hususani kwa walioko katika penzi au marafiki imesababisha wengi kuachana au mahusiano baina yao kuwa butu.
Kujua jinsi ya kuwasiliana ni kama vile kumjua wakati gani mpenzi wako amekasirika na wakati gani anafuraha, kujifunza kuzisoma maana zilizo fichika ambako mwingine hawezi kuziona (Reading behind the curtain). Kuweza kusoma maana hata katika mazungumzo yasiyo ya mdomo (nonverbal), kufahamu bayana kuwa nini humkasirisha na nini humfurahisha.
- Unyenyekevu
Hapa tunamaanisha uwezo wa kushuka na kukubali madhaifu yako bila kung’ang’anizwa, Kunyenyekea kusikosababishwa na hofu bali penzi hata katika nyakati ambazo mazingira yanaonyesha kuwa haki iko upande wako. Ni vema kujuwa kuwa unyenyekevu ni adui mkubwa wa usawa wa kijinsia. Unyenyekevu pia ni adui mkubwa wa mfumo dume.
- Kuwa muelewa (understanding)
Usiwe wakati wote unajaribu kukwepa lawama.
Usiwe wakati wote unajaribu kutafuta vigezo vya kuthibitisha katika kila
unaloelezwa au kuambiwa.
- Uwezo wa kusamehe na kukubali kusamehewa
Hiki ndicho kipimo pekee cha kukuwezesha kutofautisha penzi la kweli na lile la uongo
Kama hautaweza kusamehe (pasipokujali ninini umefanyiwa) basi hauna pendo lakweli.
MAMBO HATARI KWA WANAOINGIA KATIKA MAHUSIANO
- Epuka kuhusiana na mtu wa imani tofauti. Kumbuka Imani inauhusiano mkubwa sana na hisia zako kwa hiyo waweza kujikuta unaumia zaidi.
– Usitazamie kumwokoa mwenzako ili uoane naye. Staili hii mara nyingi imeitwa PCM (Preach Convert Marry)
- Epuka mafunuo maana mafunuo hutokea katika vyanzo vitatu, Kwa Mungu, Kwa ibilisi na Kutoka katika hisia au nafsi zetu
- Usitegemee sana vigezo vya nje (fakamavile sura, mwendo, mavazi, umbile n.k.
- Ingawa elimu ni msingi, ni hatari kuitegemea iwe ndio kipimo chako.
- Usitegemee maoni ya watu wengine, kumbuka kila mtu ana hisia na matakwa yake.
- Kujua maisha na mwenendo wa mtu huko awali ni muhimu ila mambo ya kabila na ukoo yasiwe msingi sana kwako.
- Kamwe usichaguliwe, au kupendekezewa mchumba au mke, waweza kuja kuwalaumu wengine
- Umri ni muhimu ila sio msingi wa kuchagua mwenza
- Usitoe maamuzi kwa kuangalia upendo wa nje, huu una hisia nyingi zisizo rasmi kuliko upendo wa ndani. Ni rahisi mtu kuweza kuwa “msanii”
ZINGATIA HAYA
- Tafakari nini hatima ya mahusiano yenu; Je ni ili kujifurahisha tu? Je ni katika kutafuta msaada wa kimasomo? Je ni ili kuwapamoja katika mitoko? Je ni katika kumuandaa mwenza wa maisha? Au ni mchungaji na kondoo wake wa kiroho?
- Jifunze kumuandaa mke/mume katika ulimwengu wa roho kabla na mapema, usisubiri kumuona kwa macho ya nyama.
- Maanisha unaposema “ngoja niombe au tuombe” na pia maanisha unaposema “Mapenzi ya Mungu yatimizwe”
UNAFANYA NINI UNAPOTAKA KUOA AU KUOLEWA
- Tengeneza mahusiano mazuri na wengine, panua wigo wa mahusiano kwa wengine sio tu wa kazini kwako au kanisani kwako.
- Ruhusu urafiki wako ujengwe katika misingi ya Imani.
kukua kwa urafiki wenu kuende sambasamba na kukua kwenu kiimani na
kijamii.
- Amua ni aina gani ya ndoa unahitaji kuwanayo Mfano. Kikristo/kisheria/kimila/, au kuishi na mwenza tu kirejareja.
- Fahamu mambo ya kimila au kiutamaduni yahusuyo ndoa baina yenu.
Msiishie kusema sisi hatuamini mila na jadi, sisi tuna mwamini Mungu,au
sisi ni wakisasa zaidi
YAKUPASA UOANE NA MTU WA NAMNA GANI
- Mtu unayeendana naye kiimani
- Mtu ambaye unaweza kumkubali na unaweza kujivunia.
- Mtu anayekuvutia kutokana na pendo sio kutokana rehema au fadhila
- Mtu ambaye ukotayari kumfia
- Mtu uliyekotayari kujivunia wakati wowote na mahali popote
- Mtu anayeweza kukufanya ujisikie na kujivunia jinsia uliyonayo
KANUNI
- Anza na endeleza mchakato mzima kwa kumshirikisha Mungu
- Tafuta, ila pima ushauri toka kwa wengine
- Angalia mazingira na hali inayokuzunguka na ujiulize kama ukotayari kuingia katika mahusiano yanayo tazamiwa kuwa ndoa baadaye
- Tumia pia akili yako ya kuzaliwa.
- Hakikisha mnavitu vya kufanana, kutofautiana sana huleta misuguano maumivu ya moyo, ndoa nia kituo cha furaha sio masononeko
NAWEZAJE KUMTOKEA/KUJIWAKILISHA KWA NINAYE MPENDA
- Kuwa wazi na mkweli
- Lenga kusudi lako,
- Maanisha
Na. Dr. Chris Mauki
Social, Relationship & Counseling Psychologist