PICHA: TALK YA DR. CHRIS MAUKI KWA WANAFUNZI WA FORM 5 & 6 ILIYOANDALIWA NA GLOBAL EDUCATION LINK: 23.04.2018

Dr. Chris Mauki leo alipata nafasi ya kuongea na wanafunzi wa kitado cha tano na sita kutoka shule ya secondary Pugu pamoja na wanafunzi kutoka shule ya secondary Benjamini Mkapa kuhusu masuala mbalimabli yanayowahusu wanafunzi kwa ujumla, ikiwa pamoja na nini wafanye ili kufanikisha ndoto yao ya kufaulu kwenda chuo kikuu, wasome nini wakiingia chuo kikuu, (Ni nini hitaji la soko la ajira kwa sasa),  ni changamoto zipi wanaweza kukutana nazo watakapokuwa vyuoni. Na je watakapo maliza masomo yao wajiandae vipi na changamoto za soko la ajira.  Wanafunzi wakimsikiliza Dr. Chris Mauki. Dr. Chris Mauki akiwasihi wanafunzi kuwa na taarifa muhimu kwa kile ambacho wangetamani kusoma wakiwa chuo kikuu. Akasisitiza kwamba kuna baadhi ya wanafunzi ambao wamesoma kozi chuo kikuu na baada ya kumaliza wakagundua kwamba kile walichosomea hakina soko au kina ushindani mkubwa katika kupata kazi au haikuwa passion yao, walifuata tu mkumbo.  Dr. Chris Mauki akitolea ufafanuzi juu ya umuhimu wa kijana au mwanafunzi kuwa na Role model ambaye atakuwa kama kioo  katika, elimu, kazi, na maisha kwa ujumla. Akawasihii wanafunzi kuwa na watu wanaowajenga katika maisha, kifikra, na kimawazo pia na sio kuwa na role model ambao hawana mchango kifikra au kimawazo katika elimu, kazi au maisha kwa ujumla.  Kwa mahitaji ya MC katika shughuli mbalimbali za kijamii, corporate, send off, weddings na nyingine nyingi wasiliana nasi kwa 0713 407182, 0655 756959 au chrismauki57@gmail.com. Pia kama unatumia Android system download App ya Dr. Chris Mauki na unaweza kufanya booking zote moja kwa mojaDr. Chris Mauki. An expert in Relationships, Social and Counseling Psychology. Lecturer in Psychology: UDSM. Inspirational & Motivational speaker. Family man


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *