SABABU YA 4 HADI YA 7: NINI KINAWAFANYA WANAUME KUWAKIMBIA WAPENZI WAO??

arguing 2

SABABU YA 4 HADI YA 7: NINI KINAWAFANYA WANAUME KUKIMBIA MAPEMA AU KUKWEPA KUJICOMMIT KWA MPENZI HUSUSANI SIKU ZA MWANZO WA MAHUSIANO.
(Hitimisho la talk yangu ya jana katika Leo Tena ya Clouds FM, sababu ya 1 hadi 3 nilizitoa Jumanne iliyopita)
4. Wanapoona au kugundua dalili za kutawaliwa au kukaliwa

5. Wanapoona ukaribu au utegemezi mkubwa wa wazazi au ndugu zako
Hapa yawezekana bibti anategemea asilimia 100 nduguzake au wazazi wake, hafanyi kitu hadi aulize kwao, kila akiongea haachi kumtaja babayake au mama yake au ndugu zake. Au inawezekana binti ndio anategemewa 100 na ndugu ay wazazi wake, kaka akiona picha hii anaona mzigo mkubwa ujao mbele hivyo anaweza kujiandaaa kusepa.

6. Wanapogundua ugumu au matatizo fulani kwenye tendo la ndoa
Mfano; unene au uzito wa mwili asiouweza au asioupenda, changamoto za kwenye maumbile ya sehemu za siri, harufu za kudumu asizoweza kuzistahimili, mazoea mabaya asiyoyapenda kwenye eneo hilo. Uchafu wa kudumu asioweza kuustahimili nk.

7. Akigundua unamtoto/watoto au uliwahi kutoa mimba
Akigundua uliwahi kutoa mimba kwake ni mashaka ya labda kutokuja kupata mtoto. Akigundua au kuona una mtoto/watoto kwake ni mashaka ya kubeba mzigo ambao haukumstahili.Dr. Chris Mauki. An expert in Relationships, Social and Counseling Psychology. Lecturer in Psychology: UDSM. Inspirational & Motivational speaker. Family man


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *