DARASA LA ALHAMIS na DR. CHRIS MAUKI: TOFAUTI ZA KIJINSIA NA JINSI ZINAVYOATHIRI MAHUSIANO YETU. PART 2


Wanawake wanachosema juu ya wanaume

·         Wanaume hawawezi kuzielezea hisia zao vyakutosha

·         Wanaume hawawezi kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja, lazima kwanza waache hiki ili kufanya kile, ni ngumu kuongea na mpenzi wako wakiume akiwa anaangalia soka, labda azime luninga kwanza au usubiri mpira upoe kidogo ndio akupe sikio lake

·         Wanaume hudhani kila mara wao huweza kufanya mambo kiufasaha zaidi wakati ukweli ni kwamba hawawezi

·         Wanaume sio wasikilizaji wazuri, wao wakati wote hujitahidi tu kushuhulikia matatizo yetu.

·         Wanaume ni watu waajabu sana, tunawashangaa kwanini hawafurahii manunuzi na kutembelea kwenye maduka

·         Wanaume wanatatizo katika kufikiri kwao kwamaana wakati wote wanachokiwaza ni tendo la ndoa tu, kama vile hakuna kitu kingine cha kufikiria.

Wanaume wasemavyo kuhusu wanawake

·         Wanawake wanahisia laini mno, na machozi yao yako karibu sana, kitu kidogo tu  wanalia.

·         Wanawake wana maneno mengi sana wakati sisi hatuna muda wala ladha ya kusikiliza vyote wanavyojaribu kutuambia, tunamambo mengi sana kichwani. Pia wanapoongea hukuza sana mambo tofauti na uhalisi wakile wanachokiongea

·         Wanawake huumizwa haraka sana hata na kitu au neno ambalo ni dogo na wala usingetegemea aumie, yani ni kamavile hawatakiwi kutaniwa.

·         Wanawake wanachanganyikiwa sana wanapokuwa katika manunuzi, hatakama hawana hela watatumia muda mrefu kuzunguka na kuangalia vitu vingi, kama huna hela ya nini kutumia muda mrefu kuulizia vitu?

·         Ni ngumu sana kuwaamini wanawake kwasababu hawachelewi kubadilisha maamuzi yao na msimamo waliouweka, leo atasema hili kesho amebadilika anasimamia kwingine kabisa.

·         Wanawake hutoa hitimisho katika jambo bila hata kuwa na uhakika au maelezo ya kutosha, wao huhitimisha jambo kwa vile wanavyowaza mawazoni mwao sio kutokana na uzoefu au taarifa za kuaminika au ushahidi fulani. Kwamfano; amekupigia simu mara tatu na haikupokelewa, badala ya kufikiri sababu azidi ya moja yeye atapeleka mawazo yake kuamini kwamba ulikuwa ukobize na mwanamke, kwahiyo atakapokuuliza atakuwa tayari anahasira na mwaweza kugombana tena kwa kitu ambacho wala hakina kichwa wala miguu.

·         Wanawake hudhani kwamba sisi wanaume tunauwezo wa kuzisoma fikra zao wakati hatuwezi, tunatamani watuambie vile wanavyohisi na vile wanavyotaka mambo yawe sio kutegemea tutahisi tu na kuyafanya ili wafurahi, hatuwezi kufanya tusichokifahamu au kuwa na uhakika nacho.

Baadhi ya tofauti hizi nyingi chanzo chake ni ubongo. Jinsi ubongo wa mwanaume na mwanamke ulivyo tengenezwa ni tofauti sana na ni ajabu. Pande mbili za ubongo wa mwanamke zimeunganishwa zaidi na mishipa au nyaya za mawasiliano kuliko ilivyo kwa ubongo wa mwanaume, mishipa au nyaya hizi (waweza kutafuta na kuangalia picha za ubongo) huruhusu mawasiliano ya kasi na kwa urahisi kwa ubongo wa mwanamke tofauti na mwanaume, mawasiliano haya ndani ya ubongo humuwezesha mwanamke kuwa na uwezo mkubwa katika mambo mengi ikiwemo uwezo wakufanya mambo mengi kwa wakati mmoja na yote yakaenda sawa.

Tofauti katika tendo la ndoa “Sexual differences”

·         Maranyingi wanaume wameonyesha kupenda na kutamani zaidi  kufanya tendo la ndoa hata kama tendo hilo halitowafurahisha sana wapenzi wao wa kike, hili lina sababu nyingi zikiwemo za kibaiolojia na kimaumbile pia. Najua kuna baadhi ya wanawake katika mahusiano yao wao ndio wameonekana kutamani sana tendo la ndoa kila mara lakini taarifa hizi ni chache ukilinganisha na zile za wanaume.

·         Wanaume hufikia kileleni ‘orgasm’ kwa haraka au mapema zaidi wakati wa kufanya tendo la ndoa. Jambo hili limesababisha misuguano mingi katika mahusiano mengi ingawa wanawake wengi hawakotayari kuwa wazi kwa wapenzi wao kuonyesha kutoridhika kwao na kubakia kuumia moyoni na kisirisiri tu. Utakubaliana na mimi kwamba miaka ya karibuni kumekuwa na wimbi kubwa sana la dawa, vyakula au vinywaji vinavyouzwa vikisemekana vinasaidia mwanaume kutokufikia kileleni mapema, biashara hii imepata umaarufu mkubwa kwasababu ya ukubwa wa tatizo lenyewe. Matokeo ya uhalisi huu wa wanaume kufikia kileleni mapema kuliko wapenzi wao wa kike umesababisha pia baaadhi ya wanawake kujifanya wamefika kileleni wakati wa tendo hilo wakati hawajafika ‘fake orgasm’ hii yote hufanywa ili tu kumridhisha mwanaume au kutomfanya ajisikie vibaya kwamba ameshindwa kufanya kazi yake kisawasawa. Kumekuwa pia na sababu tele za kujitetea toka kwa wanaume, wengine wakisingizia uchovu, msongo wa mawazo, kazi nyingi, magonjwa n.k. Kwa ujumla hali yote hii imesababisha hali ya kukosa furaha baina ya wapenzi kwasababu ya kule kuto toshelezana.

·         Wanaume wanaweza na wako tayari na wala hawaoni shida kutamani kufanya mapenzi hatakama wanamachungu moyoni, mmekwazana au mmeumizana. Mnaweza kugombana na mpenzi wako wa kiume na mara hiyo hiyo mkiingia chumbani kulala anaonyesha dalili zote za kuhitaji tendo la ndoa, halafu unashangaa huyu mtu vipi? Ni kweli amekasirika, tena labda zaidi yaw ewe lakini bado mwili wake unaweka hasira katika mfuko tofauti na ule unaohitaji tendo landoa. Tofauti hii ni kubwa sana kwa wanawake ambao miili yao iko kwenye mfumo mmoja unaotegemeana katika kilakitu, mwanamke akikasirishwa na kitu fulani mfumo wake wote wamwili unasinyaa, raha ya tendo la ndoa inakwisha, mpaka asaidiwe kurudi tena kwenye hali yake ya awali ili aweze kushiriki tendo hilo. Sasa tatizo huwa linakuja pale ambapo mwanaume humfikiria vibaya mpenzi wake wa kike na kudhani anaamua kumyima penzi badala ya kusawazisha hali iliyomsumbua moyo mpenzi wake na kuhakikisha anaweka mazingira ya penzi ili wafanye tendo hilo kwa kuliwazana na kufurahishana, wakati huohuo kwa kule kulazimisha apate tendo hilo kwasababu ya kuona ni haki yake, mpenzi wakike anamshangaa sana mwanaume na kuona ni kati ya viumbe wakatili. Katika mazingira haya tafiti nyingi zimeonyesha kuwepo kwa ubakaji ‘rape’ kwa wapenzi na wanandoa wengi.

  Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *