PICHA: HARUSI YA KUFANA YA RYAN NA RESTITUTA KAMUNDE. TAR. 18.4.2015 POLICE OFFICERS MESS – OYSTERBAY

Siku ya Jumamosi ya tarehe 18.04.2015 ilikuwa ni siku ya furaha sana kwa kijana Ryan mwenyeji wa kabila la Meru la nchini Kenya na mfanyakazi wa kampuni ya simu ya Tigo aliyeamua kufunga ndoa na mpenzi wake Restituta ambaye pia ni mfanyakazi wa kampuni ya simu ya Tigo. Ukumbi wa Police Officers Mess ulikuwa ni shangwe nderemo na vifijo wakati timu kubwa kutoka nchini Kenya ilipovamia na mila za kuvutia katika kuwapokea wageni na wakwe pamoja na maharusi. Wafanyakazi wa Tigo nao walinogesha shuhuli nzima maana walisheheni kila idara katika kuhakikisha kuwa staff mwenzao anajimilikisha wife na kuhakikisha hawazi wala kufikiria kurudi nchini kwao Kenya tena. Mimi pia nilipata fursa ya kushika mpini pale kati kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa na chenye utofauti mkubwa. Ngoja nikuache uendelee na raha mwenyewe

 Nikiwa na mwenyekiti wa kamati Mr James

 Nikisimamia show nzima

 Maharusi wakijiandaa kutoa keki kwa mwenyekiti wa kamati

 Ryan aki toast glass  na wakwe zake

 Mchungaji kutoka Kenya akitoa nasaha kwa maharusi

 Baba wa biharusi akitoa nasaha, Mr.  Kedmond Mnubi ni RPC wa Ikulu ya Tanzania

 Wakati wa maakuli

 Baba wa Biharusi akiwa na mwanae mkubwa wakitangaza zawadi yao kwa maharusi, Maharusi walipewa mchele, mafuta ya kupika, mashine ya kufua, shilingi milioni moja taslim, pamoja na nyumba iliyopo Kimara (Kwa moyo huu wa upendo kama baba, mzee Mnubi naomba unikubalie niwe rafiki yako wa kudumu)

 Michuzi media team pamoja na mimi
 Mr and Mrs Issa Michuzi

Kwa mahitaji ya kuendeshewa shuhuli za harusi, sendoff na nyingine nyingi wasiliana nasi kwa 0713 407182 au chrismauki57@gmail.comLeave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *