MAMBO YA KUKUSAIDIA KUONGEZA NGUVU, HAMASA NA FURAHA KATIKA TENDO LA NDOA (KWA WANANDOA) PART II


§  Jifunze kula na kunywa vitu vipasavyo na vyenye afya, sio kila kitu kwako ni chakula na kinywaji, kuwa na kiasi. Kuna uhusiano mkubwa baina ya vyakula tunavyokula na vinywaji tunavyokunywa na tendo la ndoa.

§  Epukeni msongo wa mawazo “stress” kwasababu huathiri sana tendo la ndoa

§  Jifunzeni kuiombea “kuifanyia sala” hali yenu ya tendo la ndoa na pia kumshukuru Mungu kwa zawadi hiyo nzuri baina yenu, maana ni mpango kamili wa mungu kwa wanandoa kufurahia tendo la ndoa. Ninauhakika kabisa kama unafanya tendo hili kwa wizi huwezi kujaribu kumshukuru Mungu.

§  Zishuhulikieni hofu na maumivu yenu ya ndani ya moyo “internal pains”, msijaribu kuzifunika kanakwamba hazipo, kwasababu zitakapolipuka zitalipua mahusiano yenu pia.

§  Zungumzieni kuhusu maumivu na majeraha yenu ya nyuma “past pains” na kumuomba Mungu awasaidie kupona.Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *