JE UNAKIFAHAMU KIPIMO CHA MAHUSIANO KATIKA NDOA YAKO??


Hali halisi ya tendo la ndoa baina ya wanandoa ni kipimo halisi cha mahusiano au hali ya ndoa yao, mara nyingi tatizo lolote linapotokea ndani ya kona yoyote ya mahusiano linaweza kuathiri tendo la ndoa baina ya wanandoa husika. Ni vema ukafahamu kwamba yapo matatizo yanayo anzia maeneo mengine yamahusiano yenu na taratibu yasipo wekewa mipaka huingia kuathiri tendo la ndoa, na pia yako matatizo yanayoanzia kwenye magumu, tofauti na mapishano katika mtazamo au ufanyaji wa tendo la ndoa, na kwa haraka matatizo haya kushika kasi kama saratani na kuathiri maeneo mengine ya mahusiano yenu. Mara kwa mara ninashauri wanandoa kuwa makini kuyawekea mipaka matatizo yaliyo nje ya tendo la ndoa yasiingie na kuathiri mtazamo au utendaji wao wa tendo la ndoa na yale yaliyoanzia kwenye tendo la ndoa, wanandoa wawe na uwezo na uhuru mkubwa wa kuwasiliana “sexual communication” ili wayaongee na kuyatafutia ufumbuzi kabla hayajatapakaa kwa kasi na kuathiri maeneo mengine ya maisha – Chris Mauki.Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *