USIHARIBU MTAZAMO WA WATOTO WAKO JUU YA MAHUSIANO


Kila mtu, awe mwanamke au mwanaume huzionyesha tabia zilezile alizojifunza au kuziona zikifanywa alipo kuwa mtoto, tabia hizi ni zile tulizowaona wazazi wetu wakizifanya au wakifanyiana. Wazazi, hatunabudi kuonyesha upendo, mapenzi na kuthaminiana ili watoto wetu watoke na picha na mtazamo wenye afya kuhusiana na mapenzi na mahusiano. Kwamfano, kama baba yako alikuwa akimuheshimu na kumpenda mama yako, basi hivyohivyo kuna uwezekano na wewe utampenda na kumheshimu mama yako na mke wako. Na kama hukuwahi kuona aina ya penzi na mahusiano yenye afya toka kwa baba na mama yako, mapenzi hayo yawe kama kioo cha wewe kujiangaza, au sehemu ya kuchukua mfano wa kuigwa basi mahusiano yako kwa wazazi wako na hata mwa mwenza wako yanaweza kuwa na shida – Dr. Chris Mauki.Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *