NI BORA UKAFAHAMU KABLA HAUJATESEKA SANA


Unalalamika, unalaani, unalia na kunung’unika kila wakati na yamkini wala hujajiuliza tatizo liko wapi? Alikuoa wewe ili apate msaidizi na sio mtu wa kumfundisha vitu vya kufanya, kama angehitaji hilo basi angemtafuta mwalimu. Alikuoa akiwa na kiu ya kupata msaidizi na mtu wa kushiriki naye maisha “a companion” na sio mtu wa kumuongoza kama bosi, yeye tayari ana bosi wake huko ofisini kwake, hahitaji bosi mwingine wa nyumbani, labda hakwambii tu anavyosikia vibaya unavyomkalia kooni katika kila kitu na katika kila maamuzi. Labda hakwambii tu lakini hahitaji mtu wa kuwa kama mama yake kwenye ndoa wakati tayari ameshawahi kuwa na mama, wala hahitaji mtu wa kumsimamia kama dada yake, tayari dada zake walishaifanya kazi hiyo. Utaendelea kuumia na kuteseka sana kiakili na hata moyoni mwako kama hautofika sehemu ukaitambua nafasi yako kama mke na pia ukaitambua na kuiheshimu nafasi yake kama mume. Usikopi na kuigiza jinsi mama yako alivyokuwa anahusiana na baba yako, yamkini mama yako alikuwa anakosea na kutojua uhalisia, na labda baba yako aliamua kuwa kimya ilikuepusha shari muda upite, usidhani kwa wao kuwa pamoja muda mrefu ndio walikuwa wameshibana, fahamu uhalisia na ukweli huu na ikusaidie kuyatengeneza mahusiano yako na mumeo kwa staili na mtazamo bora. Kumbukwa kwamba wakubomoa ni wewe, na wakujenga ni wewe pia. Akili mukichwa – Chris MaukiLeave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *