DARASA LA ALHAMIS na DR. CHRIS MAUKI: IFAHAMU MISONGO YA MAWAZO INAYOTATIZA FAMILIA NYINGI (FAMILY STRESS)


Katika familia kuna stress ambazo zinasababishwa na wanafamilia wenyewe na nyingine zinasababishwa na walio nje ya familia(internal and external stressors).  Visababishi vyote hivi huwaathiri wanafamilia kwanamna moja au nyingine.

Visababishi vilivyo ndani ya familia hujulikana kama “family stressors” wakati vile vinavyotoka nje ya familia huitwa “extrafamily stressors”. Matokeo ya visababishi hivi yaweza kuwa magonjwa mbalimbali kwawanafamilia.

Ukosefu wa muda waonekana kuwa tatizo kwawanafamilia wengi, wengi huwahisana kutokanyumbani mapema asubuhi na kuchelewa sana  kurudi usiku, hakuna siku shuhuli zime pungua au kuisha. Hamna aliyetayari kumpa mwingine muda wake, si mke wala si mume, kila mmoja yuko bize, kila mmoja anajitahidi kukamilisha vingi alivyonavyo katika muda kidogo alionao.

Hali hii imeondoa amani katika familia nyingisana, nyingine hazikuweza kustahimili na kwahiyi kuvunjika.

Jinsi gani twaweza kukabiliana na hili.

Jarubu kuomba marafiki wa familia nyingine kuwasaidia katika yale wanayoweza kuwasaidia, kwamfano; jirani au marafiki wanaweza kuwasaidia kufanya manunuzi, kuwachukua watoto toka shule, kwenye mazoezi ya mpira au kuwapeleka sehemu fulani. Ikishindikana basi mwaweza kuajiri mtuambaye ataweza kuwasaidia katika shuhuli zile msizoweza kuzifanya na zisizo muhimu sana ninyi kuzifanya ili kuwaachia nafasi ya kufanya vile vilivyo muhimu. Huyu anayeajiriwa anaweza kuwasaidia shuhuli kama kufua, kuosha vyombo, kutunza bustani nk. Kipaumbele chako cha kwanza, uwe mke au mume nilazima kiwe kiwe familia yako.

Ili kuhakikisha una muda mzuri na familia yako basi waweza kupanga kupata likizo za mwezi au za mwisho wa wiki, likizo zitakazo kuweka mbali na marafiki, wafanyakazi wenzako, majukumu ya kazini, ili uweze kuweka macho, akili, na masikio yako kwa familia yako.

Wenzetu wa nchi za magharibi hupanga kwenda katika likizo za kwenda katika uvuvi, uwindaji, au kucheza katika theluji. Najua mazingira yetu ni tofauti kidogo lakini wenye mashamba au mifugo nje ya mji waweza kwenda huko. Likizo za mahotelini na katika makambi (camps) ambako watoto hupiga kambi na wazazi kushiriki michezo kamavile gofu sio muafaka sana kwa familia zinazotaka kuwa na muda mzuri kwa mambo muhimu.

Ndoa ni kazi ngumu, kutunza na kuendeleza mahusiano bora katika ndoa au katika familia ndiyo kazi yenyewe. Katika utafiti uliofanywa na David Farell umeonyesha kuwa katika wanandoa waliofanikiwa katika mahusiano yao, wengi wamekuwa wakishiriki tabia  tano kuu muhimu zifuatazo.

 1. Ukweli na uhalisi kwa mwenza wako (mke/mme)
 2. Heshima na utii kwa mwenza wako
 3. Mwenza alihesabiwa kama rafiki mkubwa, sio tu kama  mke au mme
 4.  Utayari wa kusamehe na kusamehewa
 5. Hamu ya kumfurahisha na kumsaidia mwenza.

Nimatumaini yangu kuwa wote tunahitaji kutumia jitihada zetu ili tuyafanye haya katika familia zetu.

Katika visababishi vingi vilivyotajwa humu vyaweza kuboreshwa kwa kuboresha mawasiliano baina ya wanafamilia. Tenga na tafuta muda maalimu wa kuongea na kuwasiliana bayana na wanafamilia wote, sio tu kuwa bize na kutumia muda wote kwa mamboyako mwenyewe,huu ni ubinafsi mkubwa “selfishness”. Jueni kutenganisha muda wa waajiri wenu na muda wa familia zenu, nyumbani ni nyumbani mahali kwa ajili ya familia na ofisini ni ofisini mahali kwa ajili ya mabo ya kazini “two different places”.

Familia nyingine zina siku maalum katika wiki ambayo kila mmoja helezea jinsi au pale alipoudhiwa na nini kifanyike. Weka muda wa kujua nini wanao wanafanya shuleni, nani anawasumbua na kuwaumiza( miili yao au hisia zao) kwanini na wanafikiri nini. Pata muda wa kupokea mawazo yao aktika kuijenga familia yao, wewe sio bosi wa familia, watoto nao wananafasi tene bora zaidi, fahamu ninani au nini kilicho ndani ya familia ambacho huwafurahisha, huwahuzunisha, nk.

Baadhi ya vitu vinavyosababisha msongo wa mawazo katika familia (family stressors)

 • Kuzidiwa na majukumu
 • Mmoja kutoyaelewa majukumu yake
 • Mgongano katika kuyatimiza majukumu ya kifamilia(role conflict)
 • Mapungufu katika kuyatekeleza majukumu ya mmoja
 • Ukosefu wa kupeana zawadi au vichochezi au vihamasishi pale mmoja  anapofanya vema, (suprises and motivators)
 • Mahusiano mabovu
 • Ukosefu wa fedha
 • Kutotoshelezeshwa katika tendo la ndoa

Tabia binafsi ambazo zaweza kuchangia katika kuleta msongo wa mawazo

 • Mmoja kujisikia au kujithamini zaidi ya mwezake
 • Kiwango cha juu cha hasira
 • Mmoja kuchukulia kazi yake kuwa ya muhimu zaidi ya ile ya mwenzake
 • Mapungufu katika mbinu za mahusiano, Mfano; mmoja hana tabia yakusema asante, au kutoa zawadi au hata kusema neno “nakupenda”
 • Udhaifu katika afya ya mmoja
 •  
 •  
 • USIKOSE DARASA LA ALHAMISI IJAYO AMBAPO NITAKUDOKEZEA ALAMA ZA KUJUA KUWA MSONGO WA MAWAZO UPO KWENYE FAMILIA YAKOLeave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *