INASHANGAZA SANA, NA HAIINGII AKILINI


Inashangaza sana, ni ngumu na haiingii akilini, unakuwa na mpenzi ambaye anathamini marafiki zake kuliko hata wewe, yuko radhi ashinde nao kuliko ashinde na wewe, anajisikia furaha akiwa nao kuliko akiwa na wewe, akiwa nao anazungumza kama chiriku na kucheka kama bulicheka lakini mkiwa naye kauchunaaa kama anadaiwa, kila ukimuuliza kitu yeye anajibu tu ndiyo au hapana, au anatingisha tu kichwa, no comment kabisaaa!! Sasa simu ipigwe na hao rafiki zake utamuona anavyofufuka kwa furaha na anavyoipaza sauti, unaanza kumshangaa huyu mtu vipi? Unajiuliza hivi hao marafiki wamemlisha nini? Akiwa nao anajisahau kabisaa hata nyumbani hakumbuki, Kila ukimtafuta, utasikia niko na nanihii na nanihii hapa nanihii, hembu ongea nao, sasa kwani wewe umepiga kuongea na rafiki zake au kumtaka mwenzako arudi nyumbani?? Hata hajui kwamba anawatoto na wanahitaji muda nayeye. Hivi ngoja niulize, kama mtu ana mke au mume na ana watoto nyumbani na bado marafiki zake wanachukua muda wake kuliko wale wa muhimu walioko nyumbani kwake, hivi kweli huyu mtu alipevuka na kufaa kuoa au kuolewa? au labda alikurupuka au kulazimishwa na mazingira kwenye kuanzisha familia. Jamani, wakati wote huwa nasema, kukua sio tu kuongezeka ukubwa wa viungo vya mwili bali pia kuongezeka uwezo wa kufikiri – Chris Mauki Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *