JE UNAUJUA MTEGO WA HASIRA ZA WANAUME?


Wanasayansi watafiti wamegundua kwamba japokuwa wanaume wote kwa sili ya ubongo wao wana hasira zinazohusisha fujo na ugomvi “violence”, sehemu hii ya ubongo wa mwanaume inaweza kutulizwa na mambo mawili; a) Nafasi ya mwanaume huyu katika jamii mfano cheo kazini au heshima anayopata kutoka kwenye jamii yake na b) ndoa iliyo imara, hii inamaanisha kwamba mwanaume asiye na jukumu lolote, wala cheo, kipaji au kuheshimika katika jamii na yule mwenye ndoa inayoyumba au yenye migogoro sana wananafasi kubwa ya kuonyesha hasira kali tena zenye fujo na magomvi kwa wale wanaowazunguka, hama namaanisha kwamba ukiona mwanaume unayefanya naye kazi au rafiki yako mwingine anatabia za hasira za mara kwa mara, au tabia ya fujo zisizokuwa na sababu, anza kutilia shaka mahusiano yake na mpenzi wake au na mkewe  – Chris Mauki.Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *