MWANAMKE AKIKUTILIA SHAKA, JIULIZE!!!!

  
Ni vema ukafahamu kwamba ukiona mwanamke, mke wako au mpenzi wako wa kike ameanza kukuchunguza au kukuchokonoachokonoa au kukufanyia utafiti kwenye kitu chochote au mazingira yeyote ujue anakutilia shaka katika eneo hilo. Mwanamke asiye na shaka yeyote juu yako kamwe hana haja wala muda wa kukuchunguza kwa chochote, kwahiyo ukiona unachunguzwa au kufuatiliwa sana kwenye eneo fulani jiulize kwanini, na mbona maeneo mengine huchunguzwi? Nakupa mfano, najua inasumbua sana na inaleta shida kwenye mahusiano pale mpenzi wako anapoanza kufuatilia na kuichunguza simu yako, lakini fahamu tu kwamba uchunguzi au upekuzi huu lazima unachanzo, lazima kuna shaka “doubt”moyoni mwake na sasa anaamua kuingia kazini kutafuta ukweli, hofu yake hii yamkini unaijua au huijui lakini ipo, na kule kukuchunguza sio chanzo cha tatizo ni matokeo ya tatizo. Kama asingewahi kusikia, kuona, au kugundua kama unamahusiano pembeni yake wala asingehangaika na simu yako, kwa maneno mengine, wewe ndiye uliyesababisha kuchunguzwa huko na kuwekewa mashaka. Yamkini hata hajaambiwa, au hata hajakuona sehemu ukiwa na kamchepuko, ila wanawake pia huamini sana hisia zao, anaweza kuota ndoto, au akahisi kitu kuhusu wewe na akikifuatilia anakuta ni kweli. By the way kama huna cha kuficha, wala nyendo za chinichini ya nini uogope au kuwa mkali ukichunguzwa au ukihofiwa??? Fahamu kwamba“Women always speculate when they doubt” na hata sikumoja asiye mwizi haogopi mbwa – Chris MaukiLeave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *