HIVI UNAJISIKIAJE?


Hivi unajisikiaje pale ambapo mpenzi wako anakuumiza na kukutesa moyo wako na unapokumbuka huko nyuma kabla ya kuwa naye huyo au kabla ya kuoana naye uliwahi kuwa na mpenzi ambaye aliwahi kukupenda na ukajihisi kupendwa na kuona hata wewe umependa vilivyo ingawa kwa bahati mbaya hamkuweza kuwa pamoja au kuoana. Hivi unajisikiaje unavyowalinganisha hawa watu wawili? Unajisikiaje unapoona utofauti wa lile penzi na hili ulilonalo sasa hivi, ukizingatia kwamba huyu uliyenaye ndio umeambiwa utaishi naye hadi kifo kiwatenganishe? Je umewahi kukata tamaa? Je umewahi kujuta? Je umewahi kuilaani ile siku mliyokutana naye? Na je umewahi kujiuliza swali “hivi nilitokana wapi na huyu kiumbe??? Akili mukichwa – Chris MaukiLeave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *