WAKATI UNAANGALIA MIAKA YAKE USISAHAU KUANGALIA UKUAJI WAKE WA AKILI (MENTAL AGE VS CHRONOLOGICAL AGE YA MPENZI)


Unaweza kukuta unakomaa kuangalia utofauti wa miaka yenu wewe na mpenzi wako na ukasahau kwamba kuna kitu kinaitwa mental age “ukuaji au upevukaji wa akili yake”. Mpenzi wako anaweza kuwa na miaka ya kuzaliwa mingi tu, na ukadhani kashapevuka na kuwa tayari kwa ndoa, mara mnapoanza mahusiano unakuja kugundua kwamba bado akili zake hazikustahili hata kumaliza sekondari, mawazo yake, maneno yake, marafiki anaokuwa nao, maamuzi yake na hata mitazamo yake bado ni ya kitoto. Katika hali hii unajikuta sasa wewe ndio muamuzi wa kila kitu wakati ulitegemea msaidiane kwenye mambo ya muhimu ya mahusiano yenu. Usiegemee sana kwenye miaka yake ya kuzaliwa “chronological age” ukasahau kuchunguza upevukaji wa akili yake “maturity” au “mental age”usije kujikuta unaoana na mdogo wako wa mbali sana bila wewe kujua halafu ikawa badala ya kusaidiana wewe ndio unamsaidia kwenye kila maamuzi – Chris MaukiLeave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *