JE UNAKIJUA CHANZO CHA HASIRA NA FUJO ZA WANAUME KWENYE MAHUSIANO??


Ingawa katika mahusiano wanawake na wanaume hukasirika katika kiwango cha kufanana, katika uzito wa kukasirika huko na urefu au ufupi wa hasira hizo, tafiti zinaonyesha kwamba wanaume huhusisha fujo, magomvi, kupigana na hata uharibifu “violence” wanapokuwa na hasira kuliko walivyo wanawake. (Ingawa wako wanawake wachache wenye fujo pia). Sasa labda hii itakusaidia kujua kwanini wanawake hukasirishwa sana tu lakini ni rahisi mkaongea na akapoa wakati mwanaume anapokasirishwa muda mfupi tu, tayari anakuwa kashanyanyua mkono na mtu kashachapwa vibao, ngumi, kurushiwa vitu, na akikusamehe sana basi ndiyo utaishia kutukanwa kila aina ya tusi na maneno mazito kama vile yeye kamwe hajawahi kumuudhi mtu. Ni vema wewe mwanaume ukajua kuwa sio wote wenye uwezo wa kukuvumilia hiyo tabia yako, maumivu hayazoeleki hata sikumoja, utakuja kugundua kuwa mpenzi wako alikuwa anaumia mwili na moyo pale atakapoacha kukupenda, kukuheshimu, kukujali na labda hata kukukimbia – Chris Mauki.Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *