HAPA NDIPO TUNAPOTOFAUTIANA KIHISIA


Katika kusoma tafiti mbali mbali na kupitia uzoefu nilionao katika kuongea na mamia ya wanaume na wanawake hususani wale walioko kwenye mahusiano nimegundua kwamba wanaume wanawalaumu wanawake kwa kuwa walaini na wadhaifu sana kihisia “too emotional”, wanaowaona wanawake kama watu wanaongozwa au kufanya  maamuzi yao kihisia zaidi kuliko kihalisia, wakati kwa upande mwingine wanawake nao wanawalaumu sana wanaume kwa kutokujali hisia za wake zao, kwamba kila siku wanawaumiza mioyo yao hata katika yale maeneo ya hisia ambayo wanaume hawa wanajua kuwa wanawake wanaumia. kitu ambacho wanaume na wanawake hawa hawakifahamu ni kwamba maeneo yanayoshuhulikia hisia katika ubongo wa mwanamke na mwanaume ni tofauti sana, na kama kila mmoja asipokuwa na jitihada za dhati za kumfahamu mwenzake basi kuumizana huku kutakuwa kwa kila asubuhi, mchana, jioni na hata usiku – Chris Mauki.Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *