JINSI YA KUJIWEKEA MAZINGIRA BORA YA MAFANIKIO KIMAISHA

Tunapozungumzia mafanikio binafsi tunalenga kwa upana maisha mazima ya mwanadamu. Wengi unaposema mafanikio wanaelekeza mawazo yao kwenye kuwa na fedha, nyumba, magari na utajiri. Mafanikio ya kweli ya binadamu yanahusisha maeneo   kama  mafanikio kiuchumi, kama vile kuwa na uwezo wa kujikimu na kumudu garama za maisha ya kilasiku. Mafanikio ya kijamii, kamavile kuwa na mahusiano bora na wanaotuzunguka. Mafanikio ya kiroho, kama vile kuwa thabiti kwenye mambo ya kiimani. Mafanikio kihisia, kamavile kuwa na uwezo wa kujimudu kihisia nk. Ilikujiwekea mazingira bora katika kuyaelekea mafanikio yetu binafsi ni vema ufahamu na kuweza kufanya yafuatayo.
1. Tambua umuhimu wa muda na jifunze kuukomboa.
 Lazima kufahamu kuwa   kamwe huwezi kuukomboa muda kama hujui umuhimu wake. Labda tuuangalie muda katika mitazamo tofautitofauti;
Katika mtazamo wa kiimani, (kiroho), kuukomboa muda kumezungumziwa ndani ya vitabu vitakatifu kwa namna mbalimbali. Baadhi ya maanbiko yanaonyesha kuwa hata ibilisi mwenyewe anatenda kazi akijua kuwa wakati wake nimchache sana. Maeneo mengine misahafu imeeleza kuwa kati ya hatua zajuu za busara ya mwanadamu ni katika kujua umuhimu wa muda na kuukomboa.
Tukiangalia katika mtazamo wa kimaisha, watuwengi wameshindwa kufifia malengo yao waliyoyatamani kwazababu ya kufikiri kuwa muda upo tele na kwahivyo wangeweza kufanya walichokitaka wakati wowote, wakisahau ukweli kuwa muda ni mchache katika kila tunachotaka kukifanya, wenzetu waingereza wana msemo usemao “There is little time for everything”.
Kwa kutofahamu umuhimu wa muda wengi wetu wamekuwa wakifikwa na kihoro pale wanapokaribia kustahafu maana hamna walichokifanya wakiwa kazini. Maranyingi ninawashauri watu kuanza kuelekeza mawazo katika ile siku ya kustahafu mara tu unapoajiriwa, ukisubiri uwaze na kujiandaa kustahafu mudamchache kabla utajikuta unachanganyikiwa. Hii itakuwezesha kuelewa umuhimu wa muda mdogo ulionao kazini na namna ya kuukomboa ili usije kuadhirika mbeleni. Ni vema ukifahamu ukweli kuwa “Uko vile ulivyo na jinsi ulivyo kwa kulingana na vile unavyoutumia muda wako”
Tumia muda wako kuwekeza katika busara na ufahamu ,mfano; shule na kazi.     
Katika   kutafuta kuwa na busara ni  lazima kufahamu kuwa kuna wakati wa kila jambo chini ya  jua na kila jambo lahitajika kutendeka au kufanywa katika muda wake muafaka. Wengi wetu tumepata hasara katika miradi mbalimbali maana tumeshindwa kujua muda muafaka wa kuanza au kumaliza shuhuli fulani au biashara  fulani.  
2. Jifunze kuwa na malengo na kuongozwa nayo.
Mara nyingi tumejikuta tukiwa kwenye mijadala na tukilalamikia umasikini wetu kusababishwa na wazungu, nyimbo hizi zimeanza miaka mingi na kwa kadri tunavyozidi kulalama ndivyo jinsi umasikini unavyo tuzidi siku baada ya siku. Tuna pumbazika  tulilaani mabara ya ulaya na marekani kwa kusababisha umasikini wetu wakati asilimia kubwa ya watu wa mabara hayo wapo hapa kwetu miaka hii na wanazidi kufanikiwa kwa kutumia vilivyopo hapahapa na isi tukiwa hapahapa tukiwatolea macho. Mtazamo wangu niwatofauti kidogo, na ninaungana na baadhi ya tafiti ambazo zimebainisha kuwa tatizo letu kubwa limekuwa sio sana mtaji, ardhi au elimu bali ni Matumizi mabaya ya muda, na maisha yasiyokuwa na malengo.
Msingi wa malengo yetu uwe kwenye kuwekeza katika ufanisi na kuweka kipaumbele kwenye mafanikio yetu binafsi. Mipango mingi ya watu, hususan watu wa dunia ya tatu imekuwa isiyohalisi na isiyoishia kwenye mafanikio maana haikuhusishwa na muda muafaka , wenzetu wana msemo usemao “No plan without time span” yaani hakuna mpango au lengo lisilo endana na muda.
Malengo yamegawanyika katika makundi mawili, Malengo ya muda mrefu “Long term goals” na malengo ya muda mfupi “short term goals”. Malengo ya muda mrefu ni ilemipango ambayo inatuchukua muda mrefu kuitekeleza, kamavile ujenzi, elimu binafsi au ya watoto, kutafuta mwenza wa maisha nk. Malengo ya muda mfupi ni ile mipango ambayo tunaweza kuitekeleza kwa muda mfupi, kamavile kununua mavazi, kufanya usafi, kuandaa sherehe  nk. Mara nyingi inasemekana kwamba malengo ya muda mrefu yanaweza kufikiwa kiufanisi ikiwa yale ya muda mfupi yamekamilishwa vema.
Katika kuweka malengo marazote jaribu  kufikiria yafuatayo;
a)      Nini ninachotarajia kukifikia au kukipata katika lengo hili? “end product of your goal”, usijiwekee lengo tu bila kupata picha ya matokeo. Picha ya matokeo yanayoletwa na lengo hilo inamchango mkubwa sana katika kuchochea au kudumaza  ari yako kwenye kulifikia lengo husika.
b)     Ni mikakati na rasilimali gani itakayo tumika katika kulifikia lengo husika. Wengi hukaa kwenye vikao wakipanga mipango mingi ya kuanzisha miradi fulani bila kuwaza juu ya mikakati na rasilimali zitakazotumika na mara tu wanapoanza kutekeleza mipango yao hukutana na ugumu na ghafla husitisha mradi au kuuahirisha kabisa. Wewe ni shahidi wa nyumba nyingi zilizoanzwa na kusitishwa, Biashara nyingi zimefunguliwa kwa nguvu ya soda na ghafla kufungwa, watoto wengi wamejikuta wakipelekwa shule Fulani walizoziona ni nzuri na gharama na ghafla hawakumaliza mwaka wakahamishwa kukimbilia unafuu. Haya yote ni mazingira ya watu wanaojaribu kuweka malengo pasipo kuangalia mikakati au rasilimali zitakazo hitajika.
c)      Niwatu gani ambao nitawahitaji katika kulifikia lengo. Ni vizuri kujua kuwa kamwe hatuwezi kufikia malengo yetu kwa kutegemea jitihada zetu wenyewe, iko sehemu ambayo lazima utamwitaji mwingine. Wako waliojaribu kuanza mipango yao Fulani wakidhani hawatamhitaji binadamu yeyote, mara uhitaji ukatokea na kukawa na ulazima wa baadhi ya watu kuhusishwa, hapo ugumu mkubwa ukaanza. Ni vema kuishi na watu vizuri maana hujui wapi utamhitaji nani kwa kusudi gani. Wako pia walioshindwa kufikia malengo yao maana walifanya uchaguzi mbaya wa nani wa kumhusisha malengo yao. Sio kila mtu ni mtu sahihi kuhusika katika lengo lako, wako ambao unaweza kuwaambia tu waelewe nini kinaendelea na sio kushiriki, na pia wapo ambao waweza kuwahusisha katika mchakato mzima. Ugumu unakuwa kwenye hekima ya kuweza kutambua nani aelezwe pasipo kushiriki na nani aelezwe na kushiriki. Unaweza ukafanya uchaguzi mbaya na ukawa na lengo zuri kabisa lakini waliohusishwa wakaua lengo lako au kulitaifisha.
 Faida za Kujiwekea Malengo
1. Malengo hutulazimisha katika kuufikia mpango tulioupanga kwa muda muafaka.
 2. Hutuwezesha kutambua uwezo na jitihada zetu na hii hutupa ujasiri katika kulifikia lengo.
3. Hutuwezesha kuweka mtazamo wetu kwenye matokeo, na sio tu kuwa wenye bidii hewa.
 Jinsi gani ya kuutumia muda kiufanisi ili kufikia malengo yetu
1. Jitambue kama wewe ni mtu wa asubuhi, mchana au usiku. Kuna watu ambao wanaweza kufanya kazi kiufanisi wakati wa asubuhi, wengine mchana nawengine usiku, jitahidi kuweka zile kazi bora na zamuhimu katika muda ambao wewe unakuwa makini zaidi, hii itakusaidia kuukomboa muda na kuutumia kiufanisi zaidi.
2. Fahamu jinsi unavyoutumia muda wako na ni mazingira gani yanayokupotezea muda wako kwa kujua au kwa kutokujua.
3. Panga ni muda gani unafaa kufanya kazi zenye ubora na ni upi wa kufanya kazi laini mfano kusoma, kuhesabu fedha, kupasi, kufua, kupanga vitu n.k.
4. Kula chakula bora, ili kuongeza  ubora wa uwezo wa kufikiri na hivyo kutusaidia kuzalisha vilivyo bora zaidi. 
5. Ruhusu mwili na akili yako kupumzika baada ya kiwango fulani cha kazi.Wengi wetu hatuna muda wa kupumzika na hata zinapokuja nyakati za likizo wengine huziuza likizo zao kwenye ofisi au kampuni zao, tusidhani waliogundua kuwepo kwa likizo walikuwa wajinga, mwanadamu wakawaida anahitajika kupata mapumziko baada ya kiwango fulani cha kazi. Wenzetu wa nchi za magharibi wanaamini katika usemi usemao “rest is not a west of time” kupumzika sio kupoteza muda bali ni maandalizi ya muda bora zaidi wa baadae. Angalizo; hapa sizungumzii wale wanaopenda kutumia muda mrefu kupumzika tu pasipo kufanya kazi, hilo ni tatizo.
6. Epuka kulundika kazi au majukumu hadi yawe ya lazima kufanywa. Panga au jiwekee   muda wakumaliza kazi hizo “deadlines” za muda mfupi na mrefu ili kukuwezesha kumaliza kazi zako mapema. Usipende kufanya kazi katika shinikizo“pressure” kwasababu hatakama utaimaliza hiyo kazi lakini ubora au ufanisi wake hautakuwa wakuridhisha.
7. Jingenezee muda mrefu zaidi kwa ajili yako mwenyewe kwa kugawanya majukumu kwa wengine. Ningumu sana na haishauriwi kufanya kila kitu mwenyewe. Katika kugawa majukumu, ni vema tukijifunza kugawa kazi sahihi kwa mtu sahihi kwa maana yawezekana kabisa kazi sahihi ikapewa mtu asiye sahihi au kazi isiyo sahihi ikapewa mtu sahihi na kwa hali  zote hizi matokeo lazima yatakuwa mabaya.
Namna nyingine yakujitengenezea muda wa ziada katika maisha yako ya kilasiku ni kwa kujaribu kuamka mapema zaidi kuliko kawaida. Mfano, umezoea kuamka saa moja na kufika ofisini saa mbili kilasiku, na wakati huo unalalamika muda hautoshi na majukumu ni mengi, nivema ukijitahidi kuamka mapema zaidi ili ikiwezekana uwepo ofisini saa moja, Lisaa hili lililoongezeka litakusaidia sana kupunguza baadhi ya kazi na mzigo utapungua taratibu.
Wakati wowote na katika mazingira yeyote tunatakiwa kukumbuka kuwa, Mtu asiyekuwa na lengo basi analengo la kufeli na kutofanikiwa “Not having a plan is a proper plan to fail”
Na. Chris Mauki
Lecturer in Psychology
University of Dar es salaam
chrismauki57@gmail.comLeave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *