JIHADHARI MAHUSIANO YAKO YANAPOONYESHA TAA NYEKUNDU

Kama unaona mawasiliano baina ya wewe na mpenzi wako yanaelemea zaidi kwenye kuzungumzia masuala kama vile, watoto, kazi, biashara, pesa, ndugu, mashamba, ujenzi, mifugo, elimu za watoto, afya ya watoto, gesi imeisha, na masuala mengine ya nyumbani kama vile hiki kiko wapi na kile kikowapi, au labda mwenzi wako akiwa hayupo nyumbani akikupigia simu au kukutumia ujumbe anauliza tu watoto wanaendeleaje? Nyie mko salama? Hana kiu nyingine yakutaka kujua zaidi kuhusu wewe kama mpenzi wake na hisia zako, na wala wewe hauna kiu ya kutaka kufahamu zaidi kuhusu yeye anaendeleaje, hisia zake huko aliko, na kujua kama anakukumbuka au la, unaishia tu kumjibu maswali yake, “ndiyo hawajambo”!! “kila kitu kiko sawa kwaheri”!!. Ukiona mawasiliano au maongezi ya namna hii yanazidi mawasiliano baina yenu kuhusu nyie wenyewe binafsi, mahusiano yenu na penzi lenu, na pia kama muda wenu wa kuketi kuzungumza hayo mambo niliyoyataja awali unazidi ule muda wenu wa kuzungumza mambo yenu binafsi, basi kuna uwezekano mkubwa mahusiano yenu yako wodini, na inawapasa muwe macho sana na hali hii kwasababu hapo kuna mawili, aidha mahusiano yenu yakitoka wodini yaende kwenye chumba cha wagonjwa mahututi “ICU” au yakaenda mochwari “mortuary” kabisa. Haya sasa kazi kwenu kumuokoa mgonjwa wenu – Chris Mauki
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *